Taasisi ya TAMISA (Tanzania Mining industry suppliers Association) leo imefanya uzinduzi wa kamati ya masoko na mawasiliano ambayo itaongozwa na Dr Sebastian Ndege.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Dr Sebastian Ndege amewashukuru wanachama na wageni waalikwa kwa kushiriki kwenye uzinduzi huo ambao uliambatana na mipango ya mikakati ya TAMISA na Wizara ya Madini nchini.
Dr. Sebastian Ndege amesisitiza Kwa kusema kuwa “siku ya leo sio siku tu muhimu kwa TAMISA kwa uzinduzi wa kamati yetu, bali pia ni mwanzo mzuri wa mapinduzi makubwa yanayoenda kutokea kwenye ushiriki wa wazawa na Watanzania kwenye uchumi wa sekta ya madini” Click Here and Listen